Total Pageviews

Friday, June 8, 2018


Ni rahisi kutunza kuku wakienyeji
May 22nd, 2018
Na AKLEY ALEX dibbaxyakleyalex@gmail.com

Unaweza kutunza kuku wakienyeji naukawa nakipato cha uhakika, pamoja na lishe nzuri kwa ajili ya familia.
http://www.mkulimambunifu.org/wp-content/uploads/2013/01/Kuku-1-300x182.jpg
Ulishaji: Kuku wa kienyeji wanaweza kulishwa kwa kumia mahindi, mchele, na mabaki ya ugali. Vyakula hivi nilazima vikaushwe vizuri na kusagwa vizuri. Ulishaji nilazima ufanyike katika sehemu safi au kwakutumia vyombo vilivyotengenezwa maalumu kwaajilii yakulishia kuku.
Banda: 
Ø  Kuku wawe wa kienyeji au wakisasa, wanahitaji kuwa na banda nzuri kwaajili ya malazi na kuwalinda.
Ø  Wanahitaji chumba chenye nafasi ya kutosha na kinachopitisha hewa ya kutosha.
Ø  Ni lazima kuwawekea fito kwakuwa ndege hupenda kupumzika juu ya fito.
Ø  Ni lazima banda la kuku lifungwe vizuri nyakati za usiku ilikuzuia wanyama wanaoweza kuwadhuru kuku.
Ø  Ni lazima liwesafi wakati wote ilikuzuia magonjwa kama vile mdondo na mengineyo. Usitumie pumba za mbao au nguo kuweka kwenye viovyakutagia kwani huchochea kuwepo utitiri na funza  wa kuku. Inashauriwa kutumia mchanga laini.
Maji ya kunywa: 
Ø  Kuku wapatiwe maji safi. Ni lazima kuangalia marakwa mara na kuyabadilisha maji. Kamwe usiwape kuku majima chafu.
Chanjo: 
Ø  Chanjo kwa mifugo ni lazima ilikuzuia mashambulizi ya magonjwa. Magonjwa yaliyozoeleka ni kama vile Mdono, Kideri, Ndui ya kuku, nahoma ya matumbo (typhoid).
Ø  Chanjo kwakawaida hutolewa maramoja kwa kila baada ya miezi miwili.
Uwekaji wa kumbukumbu: 
Ø  Kumbukumbu zijumuishe aina ya ulishaji, namba ya uzalishaji, muda wa mwisho wa matumizi, kiasi cha malisho kwa kilasiku, idadi ya vifo, na idadi ya mayai yaliyozalishwa.
Mwanzoni unahitaji nini?
Ø  Wafugaji waliowengi wanauliza wanahitaji nini katika hatua za awali ilikuweza kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku. Hii itategemea aina ya kuku uliochagua kufuga.
·         Ni busara kuwa na vifaa muhimu vinavyohitajika na viwe katika hali ya usafi kabla ya kuweka kuku bandani mwako. Kama unaanza na vifaranga, vifuatavyo ni vifaa muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya vifaranga 200.
       I.        Tenga na utengeneze banda zuri lenye joto na hewa ya kutosha wakati wote.
     II.        Vyombo vinne (4) vyakunyweshea maji, hii nikatika wiki 2 za mwanzo na uongeze vyombo taratibu kulingana na kuku wanavyokua.
    III.        Vyombo vinne (4) vyakulishia chakula, na viongezeke kulingana na kuku wanavyokua.
   IV.        Matandazo makavu na safi, inaweza kuwa maranda au mabua ya ngano.
    V.        Pakiti moja au mbili za dawa ya Coccid (hii inapatikana katika maduka yote ya kilimo). Hata hivyo, utaratibu wa chanjo nilazima ukamilishwe.
   VI.        Chakula  kwa ajili ya vifaranga ambacho kimezalishwa na watengenezaji wanaoaminika.

No comments:

Post a Comment

Ni rahisi kutunza kuku wakienyeji May 22nd, 2018 Na AKLEY ALEX dibbaxyakleyalex@gmail.com Unaweza kutunza kuku wakienyeji naukawa...